Agano Jipya: Je,
simulizi za Injili na matukio mengine mle ndani zaweza aminika?
Neema na iwe kwenu na amani,
zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
Katika
chapisho la kwanza niliangazia kanuni inayoelezea: Kazi iwayo yoyote ile ya kiufundi lazima iwe imefanywa kwa akili na kwa
ajili ya lengo mahususi. Shabaha ikiwa kuijibu shutma toka kwa vimbelembele ati Hakuna Mungu! Sawa na ule wa Kwanza, mjadala unaofuatia unalenga kuonyesha wazi udhabiti wa yale tuyasomayo katika Biblia Takatifu. Kwanza nitakuulizeni, je ushawahi fahamu jinsi nakala za kale hudhibitishwa kuwa za kweli au ghushi? Ni ushahidi upi na vigezo vipi hutumika aidha za kisayansi, kihistoria au za kielimu kwa ujumla kutofautisha nakala hizi?
kwa mwongozo huo, tutamulika vigezo viwili ambavyo sharti vihusishwe wakati wa kubaini uhakika na uhalisi wa vitabu/nakala zinazosimulia matukio ya kale. Baada yakufahamu matakwa ya vigezo hivi vikuu, tutatwika Agano Jipya mtihani ili kubaini kana kwamba Kitabu hiki kitafuzu au kitafeli kutimiza matakwa ya vigezo husika.
kwa mwongozo huo, tutamulika vigezo viwili ambavyo sharti vihusishwe wakati wa kubaini uhakika na uhalisi wa vitabu/nakala zinazosimulia matukio ya kale. Baada yakufahamu matakwa ya vigezo hivi vikuu, tutatwika Agano Jipya mtihani ili kubaini kana kwamba Kitabu hiki kitafuzu au kitafeli kutimiza matakwa ya vigezo husika.
Kwa wengi waliohitimu najua sina haja ya kukuelezeni kwamba vigezo husika vimetambulika na kuheshimika
katika kila fani na asasi za elimu kote duniani. Lakini ili kuwatosheleza
wabishani na wajuaji ndio maana sina budi ila kusisitiza vile! Haya basi, nakala
yoyote ile inayo daiwa kusimulia matukio ya zamani ili ikubalike kuwa ni kweli na
simulizi zake sio hekaya za kubuni, lazima itimize vigezo hivi viwili vikuu.
- Sharti nakala husika iwe imeandikwa kwa muda fulani baada ya jambo husika kutendeka.
- Sharti kuwe na ekzibiti zaidi ya moja inayoshuhudia matukio yale yale.
Swala
la kuuliza hapa ni, mbona vigezo hivi viwili hutiliwa maanani na wasomi pamoja na
watafiti? Kwa kigezo cha kwanza; kwa mfano, muda mwingi
ukipita kati ya tukio na kunakiliwa kwake, mabo mengi yaweza sahaulika, kwa
hivyo simulizi husika itakuwa na upungufu mkubwa sana katika maelezo yake. Pia
huwa rahisi kuongeza mambo ya uwongo, maana labda wahusika au mashahidi walishaaga
na hivyo hakuna mhusika wa tukio lile atakayezua pingamizi.
Kigezo
cha pili; wingi wa ekzibiti kama tujuavyo huongeza uzito wa ushahidi. Kwa mfano,
wanasheria na majaji wanafahamu vema kuwa vile ekzibiti zinavyo zidi kuanikwa
dhidi ya mshukiwa ndivyo nafasi yake yakuponea huzidi kudidimia. Vile vile,
ekzibiti nyingi za nakala moja kuhusu tukio moja zikipatikana ndivyo uzito wa
jambo lile kuwa kweli hudhibitika.
Plato: Mwanafilosofia mashuhuri aliyeishi miaka ya 427-347 BCE., ndiye aliyemrithi
mwalimu wake Socrates. Simulizi "Dialogues" za gwiji huyu ambazo zimetufunza mengi kuhusu
fani ya filosofia zimeratibishwa 900 BCE. Hili ni pengo la zaidi ya miaka
elfu moja (1000) tangu kuishi kwa Plato, na kwa ujumla nakala saba (7) pekee
ndizo zipo!
Flavius Josephus: Mwanahistoria aliyeishi Mashariki ya Kati, miaka ya 37 – 100CE. Anatambulika kwa kunakili matukio mengi
yaliyohusu, uongozi, siasa, desturi na vita vya zama zile. Nakala zake za "Antiquities" kwa
ujumla ni tisa (9) na zimaratibishwa karne ya tano (5), pengo la miaka mia nne (400) tangu uhai wa
Josephus!
Agano Jipya: Nakala ambazo
zimeptikana fika sasa zimeratibishwa kuanzia mwaka125 CE., chini ya miaka mia (100) tangu
kuishi kwake Bw. Yesu Kristo! Aliyeishi miaka ya 00-33CE. Kwa ujumla kuna zaidi ya nakala elfu tano mia saba (5,700)
kwa lugha ya Kigiriki na zingine elfu kumi na tisa (19,000) katika lugha
tofauti!
- Je, ukilinganisha kazi hizi tatu tajika ni ipi iliyo na pengo ndogo kati ya kuandikwa kwake na matukio yanayosimuliwa kwenye nakala husika?
- Je, ukilinganisha kazi hizi tatu tajika ni ipi iliyo na wingi wa ekzibiti?
- Je, ukilinganisha kazi hizi tatu tajika ni ipi ya kukubalika na kuaminika zaidi?
Basi itakuwaje, mtu awaye yeyote ule
aliyetimamu na tena aliyepata kukanyaga ndani ya shule kusema ati hakuna
ushahidi wowote ule wa kuaminika kuhusu yale tunayosoma kwenye kitabu cha
Biblia na hususan Agano Jipya!
kwa mujibu wa ushahidi uliombele yetu sote, nawaulizeni; mbona hadi leo Kitabu
hiki Takatifu kinazidi kushambuliwa toka kila upande? Usikune kichwa bure,
shutma na mashambulio haya ya kila aina huwa na lengo lile-lile siku zote;
kutia ushahidi ulioko katika Biblia nzima dosari, ati kuwa Biblia Takatifu sio Neno la
Mungu, Mumba wa vyote!
No comments:
Post a Comment