HERI ALIYEMFANYA BWANA KUWA TUMAINI LAKE
Nalimngoja
Bwana kwa subira, Akaniinamia akakisikia kilio changu.
Akanipandisha
toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu
mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.
Akatia
wimbo mpya kinywani mwangu, Ndio sifa zake Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa,
Nao watamtumaini Bwana
Heri
aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake, Wala hakuwaelekea wenye kiburi, Wala hao
wanaogeukia uongo.
Ee
Bwana, Mungu wangu, umefanya kwa wingi Miujiza yako na mawazo yako kwetu;
Hakuna awezaye kufananishwa nawe; Kama ningependa kuyatangaza na kuyahubiri, Ni
mengi sana hayahesabiki.
Dhabihu
na matoleo hukupendezwa nazo, Masikio yangu umeyazibua, Kafara na sadaka za
dhambi hukuzitaka.
Ndipo
niliposema, Tazama nimekuja, (Katika gombo la chuo nimeandikiwa,)
Kuyafanya
mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni
mwangu.
Nimehubiri
habari za haki katika kusanyiko kubwa. Sikuizuia midomo yangu; Ee Bwana,
unajua.
Sikusitiri
haki yako moyoni mwangu; Nimetangaza uaminifu wako na wokovu wako. Sikuficha
fadhili zako wala kweli yako Katika kusanyiko kubwa.
Nawe,
Bwana, usinizuilie rehema zako, Fadhili zako na kweli yako na zinihifadhi
daima.
Kwa
maana mabaya yasiyohesabika Yamenizunguka mimi. Maovu yangu yamenipata, Wala
siwezi kuona. Yamezidi kuliko nywele za kichwa changu, Na moyo wangu umeniacha.
Ee
Bwana, uwe radhi kuniokoa, Ee Bwana, unisaidie hima.
Waaibike,
wafedheheke pamoja, Wanaoitafuta nafsi yangu waiangamize. Warudishwe nyuma,
watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu.
Wakae
hali ya ukiwa, na iwe aibu yao, Wanaoniambia, Ewe! Ewe!
Washangilie,
wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe
Bwana.
Nami
ni maskini na mhitaji, Bwana atanitunza. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu,
Ee Mungu wangu, usikawie. (Amin)
Zaburi 40
No comments:
Post a Comment