SI TANGAMANE NA WAASI MUNGU
Si
Tangamane Na Waasi Mungu
Vikaragosi wa Jehanamu,
daima mcha Mungu kwao adui,
Kwa matusi na majitapo
hushtumu, wakijidai ati hao ndo wasomi
Wakijiona wenye hekima
kumbe n'pumbavu, yao adhabu wajibebea kifuani
Si tangamane na waasi Mungu,
uzao wa Lusifa malaika aliyelaaniwa kawa shaitwani!
Mcha Mungu zidisha dua, matendo na mwenendo mwema ziwe kwako pete na mkufu
Usimwonee masikini na umkumbuke
mjane na yatima, kauli mbiu toka kwake Mungu
Tenda wengine utakavyo kutendwa, mhimidi Mola wako baraka takujazia maradufu
Si tangamane na waasi
Mungu, uzao wa Lusifa malaika aliyelaaniwa kawa shaitwani!
Epukeni gadhabu na hamaki za Mumba, kwa kutia akili na uadilifu katika kazi zenu
Rahmani ni mwingi wa
wema na fadhila, usipuuze rehema zake kwa kujizulia hukumu
Kiburi kikikuongoza
mwisho tafedheheka, dhambi ikiwa yako fahari mwisho Jehanamu
Si tangamane na waasi
Mungu, uzao wa Lusifa malaika aliyelaaniwa kawa shaitwani!
Bado muda upo
wakubadili yako njia, mgeukie Masihi ni mwepesi wa kurehemu
Kila uchao huzifanya upya zake
rehema, n'mwingi wa neema haweki akiba ya kosa zetu
Jisalimishe kwake katu
hatokukataa, hakuna linalomzidi usitie shaka muamini tu
Si tangamane na waasi
Mungu, uzao wa Lusifa malaika aliyelaaniwa kawa shaitwani!
No comments:
Post a Comment